Hata ukiwa mgonjwa au safarini, fuatilia fedha, stock, oda na wafanyakazi wako kutoka popote ulipo. Ripoti inakufikia WhatsApp kila siku — bila wewe kuwepo dukani.
Biashara ambayo haiwezi kujiendesha bila wewe, si biashara bali ni ajira uliyojiajiri mwenyewe.
Inafaa biashara ndogo za aina yoyote — duka, hoteli, lodge, minisupermarket, famasi, genge na nyinginezo — kila moja ikishughulikia kazi ya kila siku ya biashara yako.
Weka float ya asubuhi, ingiza mauzo na matumizi. Ukitumia zaidi ya unavyopata, unaonywa papo hapo.
Orodha ya kazi za kufungua na kufunga — mahudhurio, usafi wa sakafu na rafu, muda wa kufungua.
Mmiliki anaona oda zilizolala, oda mpya zilizoingia, na mahitaji ya kununua ya siku hiyo — yote sehemu moja.
Inawakumbusha na kufuatilia kama wafanyakazi wamepost WhatsApp Status ("Tupo Wazi") na Instagram kila siku.
Inawahimiza wafanyakazi kutembelea wateja wapya, kupiga simu wateja wa siku zote kujua status ya oda yao, na kuomba oda mpya.
Weka kiwango cha chini kwa kila bidhaa (pcs, kg, lita) — unaonywa kabla haijaisha kabisa.
Muhtasari wa siku nzima — fedha, stock, wafanyakazi — kwa picha za ushahidi, tayari kutumwa.
Faili moja, kwenye simu yako. Data haiendi kwa mtu mwingine mpaka wewe mwenyewe utume.
Zana inakuja kama faili moja unalolihifadhi kwenye simu — hakuna app store, hakuna usajili.
Kila mtu anaingiza taarifa zake kwa simu yake mwenyewe, hata kama hamko sehemu moja.
Fedha, stock, wateja, oda, masoko, kazi za ufunguzi na ufungaji — kila kitu kinaingizwa unavyoendelea na siku.
Mwishoni mwa siku, muhtasari mmoja unatumwa kwako moja kwa moja — hata kama uko mbali na duka.
Inafanya kazi kwenye simu bila mtandao. WhatsApp inahitajika tu wakati wa kutuma ripoti.
Hakuna seva ya nje inayohifadhi taarifa za duka lako bila ridhaa yako.
Imejengwa kwa lugha na mazingira ya wafanyabiashara wa Tanzania.
Chagua mpango unaokufaa — lipa kila mwezi, au lipa miezi 6 mara moja upate bei nafuu.
Lipa mwezi mmoja mmoja, jisitishe wakati wowote.
Lipa TZS 120,000 kwa miezi 6 — unaokoa TZS 60,000.